Friday, June 21, 2013

Kim Kardashian NA Kanye West WAMPA MTOTO WAO JINA LA "NORTH WEST"


Kim Kardashian na Kanye West, wampatia mwanao jina la North West na sasa cheti chake cha kuzaliwa chaptikana, kinaonesha hakina jina la katikati na mtoto amezaliwa jumamosi, 15/06 katikka hospitali ya Cedar Sinai pande za  Beverly Hills, California. 

CLICK HAPA KUANGALIA BIRTH CERTIFICATE YENYEWE!!!



Wednesday, June 19, 2013

RIHANNA AMPIGA SHABIKI NA Microphone KWENYE SHOW... Angalia hiyo video hapa!!!!



Rihanna alikua nchini England jumatatu wakati akifanya show katika mji wa Birmingham, alilazimika kumpiga shabiki na mic alifanya hvyo baada ya watu kumsonga sana baada ya kushuka stejini na kupita karibu na mashabiki na shabiki mmoja alikua akimvuta hali iliyopelekea rihanna kumsukuma kutumia mkono aliokua maeshika mic.

DRAKE AFUNGUKA KUHUSU BIFU LAKE NA CRIS BROWN JUU YA RIHANNA

Drake amefunguka kupitia magazine la GQ la nchin marekani ambalo linatoka mwezi wa july mwaka huu, Drake ameliambia gazet hilo maneno haya hapa
“I don’t want my name to be synonymous with that guy’s name. I really don’t. I wish we could sit down, just like you and me are right now, and talk it out man-to-man. But that’s not going to happen.” 
Na kipindi cha nyuma kidogo drake ameshawah kusema
“I’m not confrontational, but if someone challenges, I’m not going to back down.”
Hii inaonesha wazi kuwa bifu kati yake na brizzy kuna utata katika kulimaliza, na alipo ambiwa afunguke zaidi drake amesema  “Like, it gets really dark.”
Gazeti hilo maarufu linatoka June 25.

Tuesday, June 18, 2013

DIAMOND MBIONI KUACHIA NYIMBO MPYA!!!!

Hii ni picha ambayo tumetumia kama evidence na maneno yake amabyo ameandika baada ya kupost hii picha instagram leo, maneno hayo ni
" Na nina wivu sikatai, Maana uchugu wa mapenzi naujua... So usije nilaghai, nikaja kunasa ukanizingua"
ukisoama huo mstari utagungua kuwa ni sehemu ya wimbo mpya, bado hajaongea chochote, endelea kufatilia blog yetu kwa update zaidi.

MTANZANIA nominated KUTOKA WIKI IJAYO BIG BROTHER,,, Soma hapa

NANDO- TANZANIA
 BOLT- SIERA LEONE
 BETTY- ETHIOPIA
 ELIKEM- GHANA
 MOTAMMA- BOTSWANA
 ONEAL- BOTSWANA
NATASHA- MALAWI

Hizi ni picha za washiriki wa bigbrother ambao wamekuwa nominated kutoka wiki ijayo endapo watapata kura chache, katika list hiyo mtanzania Nando naye yupo katika hatari ya kutoka hivyo onyesha upendo kwa kumpigia kura mara nyingi uwezavyo ili abaki katika shindani na kutuwakilisha vizuri kwa kupeperusha bendera ya Tanzania katika shindano la bigbrother.

Unaweza ukapiga kura kutumia simu kwa njia ya meseji , au online. zaidi temebelea website yao www.bigbrotherafrica.dstv.com 

Sunday, June 16, 2013

WAJUE WASHIRIKI WAWILI WALIOTOKA BIG BROTHER LEO!!!

 Biguesas
Neyll

Hawa wote ni washiriki kutoka nchini angola, safari yao imefikia tamati leo baada ya kutoka katika sshindano kwa kupata kura chache. Kutokana na hivyo bas ANGOLA wanabaki bila mshiriki katika nyumba hyo.
Watanzania tuwaombee wasiingie katika danger zone wiki hii na kupigiwa kura za kutoka na kama itatokea hvyo Watanzania tuwapigie kura wenzetu wazidi kutuwakilisha vyema. unaweza kuchek matukio na kupiga kura kupitia www.bigbrotherafrica.dstv.com 

SOMA ALICHO SEMA LADY JAYDEE KWA MASHABIKI WAKE KUPITIA TWITTER LEO



Saturday, June 15, 2013

OMMY DIMPOZ AOMBA MSAMAHA, soma alichosema hapa!!

HIKI NDICHO ALICHO ANDIKA OMMY DIMPOZ KUPITIA ACCOUNT YAKE YA FACEBOOK

Samahani tena sana na sitawacha kuomba msamaha,nimekubali makosa na hivi sasa naelekea nyumbani kwao kuomba msamaha kwa familia na nitue kwa vituo vya radio kuomba msamaha kwa wabongo na wote niliowaudhi.samahani sana na nakubali mimi si mtu bila nyinyi na sikuongea kuhusu legend Ngweir kwa ila mbaya.One Love.

LADY JAYDEE AFUNIKA MBAYA KWA IDADI YA WATU SHOW YAKE YA JANA,, ANGALIA PICHA HIZI..!

 GETINI WATU WAKIINGIA NDANI
 GETINI
 UKUMBI KWA NDANI KABLA WATU HAWAJAINGIA
 HAPA NDANI SHOW INAENDELEA
 MASHABIKI WA LADY JAYDEE
 LADY JAYDEE AKIIMBA YAHAYA
JIDE ON STAGE

MWANA FA "THE FINEST" SHOW!!!

 Mwana FA akiperfom
 Hapa ni kabla ya kuingia ukumbin, kushoto ni LINA SANGA
 mwana fa kama zamani
Lina, Mwana Fa & Maua, 
 Dully na Mwana Fa
Baadhi wa mashabiki


hizi ni baadhi ya picha za kwenye show ya Mwana Fa "THE FINEST" amabayo ilifanyika jana 14/june/2013
Kama tunavyojua kuwa kulikua na kutokuelewana kati ya mwana fa na lady jaydee sababu ya show zao kuwa siku moja hali ambayo imepelekea watu kutaka kufahamu je nani ataibuka na washabiki wengi kwenye show yake, baada ya show zote kufanyika ukweli ni kwamba mwana fa amefunikwa na mwanadada lady jaydee kutokana na idadi kubwa ya watu walioenda kutazama show yake....

Friday, June 14, 2013

BAADHI YA PICHA ZA WASHIRIKI WA BIG BROTHER TOKA TANZANIA NDANI YA MJENGO

 Nando (kushoto) siku ya evection. #day3
 Feza na Huddah
 Nando (kulia) na Motamma (kushoto)
 Feza Kessy
 Nando na BIMP1
FEZA

NEW TRACK: LADY JAYDEE - YAHAYA

New hit: G LUCK FT JOHN LOVE- UULIZE_MOYO

New Track: Q chillah - Beautiful

RATIBA YA MAZISHI YA LANGA

RATIBA YA MAZISHI YA LANGA KILEO: Ratiba ya mazishi ya ndugu yetu Langa Kileo itakuwa kama ifuatavyo, msiba upo nyumbani kwa wazazi wa Langa maeneo ya Mikocheni nyuma ya Hosp ya AAR zamani kulikuwa na ofisi za Benchmark Production. Mwili wa marehemu utaagwa siku ya Jumatatu majira ya saa 7 mchana na baada ya hapo mwili utaelekea makaburi ya Kinondoni kwa mazishi majira ya saa kumi alasiri.

Thursday, June 13, 2013

VIDEO MPYA YA VANESSA MDEE - CLOSER

PHOTO: OUR BEST FAN

Full Name: Generose Kibonde
a.k.a Gene rozay
Nationality:Tanzanian
Occupation: Student @IRDP
Relationship: In relation
Religion: Christian
Live in Dar es salaam

NIKI WA PILI NA G NAKO WAMEHAIRISHA SHOW YAO KUPISHA MSIBA YA LANGA


hichi ndio alicho tweet niki wapili leo

HISTORIA FUPI YA LANGA..... ISOME HAPA


Langa alishiriki shindano la Pop Star akiwa na wenzake wengine wawili Sara Kaisi 'Shaa' na Witness Mwaijaga 'Witness' na waliunda kundi lilioenda kwa jina la Wakilisha.

Wakiwa na kundi la Wakilisha Marehemu langa na Wenzake hao walitamba sana kwa nyimbio mbili za 'Unaniacha Hoi' na 'Kiswanglish'.
Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.

 Baada ya hapo Langa alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’ ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.

Kibao chake hicho cha  'Matawi ya Juu' na video ya wimbo huo ikaingizwa katika mashindano ya MTV Base na baade kushinda tuzo ya Kisima nchini Kenya.

Aliwahi fanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini kama Fid Q na nje ya nchi kama vile kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin Wyre).

maisha ya Langa kimuziki yalianza kuporomoka pale alipoachia albam yake ya 'Langa' na kushindwa kuuza baada ya kukataliwa na wasambazaji na kuamua kujiingiza katika maisha ya uteja ya utumiaji wa madawa ya kelevya.

Baada ya jitihada za familia yake aliweza kuondoka katika maisha hayo ya uteja na alipo toka aliachia nyimbo za 'Bombokiata' na 'Mteja Aliyepata Nafuu'.

Langa alizaliwa mnano mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.

Alipata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Olympio na baade  Sekondari ya Loyola, zote za jijini Dar es Salaam.

 Akiwa kidato cha pili alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.

MATAWI YA JUU BY LANGA

BREAKING...!!!! LANGA AFARIKI DUNIA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Langa Kileo, maarufu kama LANGA amefariki dunia leo hii baada ya kuugua maralia kali ambayo ikapelekea hali ya kupelekwa Hospital ya taifa muhimbili ambapo umauti umemkuta. Endelea kufatilia blog yetu kwa habari zaidi kuhusu kifo chake.
#RIP LANGA

Monday, June 10, 2013

H BABA, AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA FLORA MVUNGI.,, NOORAH ANE AFUNGA NDOA YAKE HUKO SHINYGA. Angalia picha zao hapa!!!

 H. baba na flora mvungi
Flora akimnywesha maji Mumewe

 Noorah na mkewe

Show ya MWANA FA ni siku moja na show ya LAD JAYDEE, Ijumaa tar 14 June

Baada ya mwana fa kuhairsha show yake, THE FINEST sasa ametangaza rasmi kuwa itafanyika Tarehe 14 june, ni siku hiyo hiyo ambayo lady jaydee alitangaza kuafnya show yake ya kutimiza miaka 13 katika muziki, kutokana na hali hiyo kumeonekana kuna utata kwa mwandada lady jaydee baada ya kuanza tweet, tweet ambazo zinaonesha kutokubaliana na hali hyo na kusema kuwa ni mpango wa kumuharibia show yake.

HAWA NDIO WALIOKUA NOMINATED KUTOKA WIKI HII BIG BROTHER

 ANNABEL- KENYA
 BIGUESAS- ANGOLA
 NEYLL- ANGOLA
 NATASHA- MALAWI
POKELLO- ZIMBABWE

Kama ilivyokawaida mwenye kura chache ndio atatkae aga shindano hilo wiki ijayo,Mpigie kura mshiriki umpendae mara nyingi uwezavyo ili aweze kubaki ndani ya mjengo.

BAADHI YA PICHA ZA KAMPENI YA UCHAGUZI WA RAISI WA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO CHA MIPANGO DODOMA

Hizi ni baadhi ya picha wakati wa kupiga kampeni katika hostel ya mapambazuko, Miyuji Campus.
Wanafunzi wakicheza mziki na kumshangilia mgombea
 Mwanadashost Diana akifanya yake
 Choya man mzee wa viduku
 Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza mpambe wa mgombea
 Mmoja ya wagombea, akinadi sera zake
Gari la muziki, lilitumika kupiga kampeni