Monday, June 10, 2013

STAR TV YAZUIWA KUJITOA STAR TIMES

Baada ya kituo cha television cha star tv kutangaza kujitoa kurusha matangazo yao kupitia king'amuzi cha star times, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imesema sheria na leseni hairuhusu kuchukua hatua hiyo, na kwamba chanel 5 za kitaifa zinapaswa kuoneshwa bure kwenye ving'amuzi.
Hata hvyo TCRA itakutana na Star tv na Star times leo ili kujadili suala hilo na hatua za udhibiti zichukuliwe ili kuwezesha wananchi kupata haki yao ya msingi ya kupata matangazo bure kupitia chanel hiyo.
Uchunguzi uliofanywa na blog hii ni kwamba hadi sasa chanel hiyo hairushi vipindi vyake kupitia star times kuanzia jana.

No comments:

Post a Comment