Langa alishiriki shindano la Pop Star akiwa na wenzake
wengine wawili Sara Kaisi 'Shaa' na Witness Mwaijaga 'Witness' na waliunda
kundi lilioenda kwa jina la Wakilisha.
Wakiwa na kundi la Wakilisha Marehemu langa na Wenzake hao
walitamba sana kwa nyimbio mbili za 'Unaniacha Hoi' na 'Kiswanglish'.
Baadaye Sarah Kaisi (Shaa) alijitoa. Lakini Langa na Witness
walifyatua kibao cha ‘No Chorus’.
Baada ya hapo Langa
alifyatua kibao chake cha kwanza akiwa mwanamuziki binafsi, ‘Matawi ya Juu’
ambacho Dj John Dilinga (JD) aliwahi kuelezea ni moja ya kazi nzuri kutoka
kwake, licha ya dosari za matumizi ya lugha.
Kibao chake hicho cha
'Matawi ya Juu' na video ya wimbo huo ikaingizwa katika mashindano ya
MTV Base na baade kushinda tuzo ya Kisima nchini Kenya.
Aliwahi fanya kazi na wasanii mbalimbali wa nchini kama Fid
Q na nje ya nchi kama vile kundi la Necessary Noise, Naaziz na Wyre (Kevin
Wyre).
maisha ya Langa kimuziki yalianza kuporomoka pale alipoachia
albam yake ya 'Langa' na kushindwa kuuza baada ya kukataliwa na wasambazaji na
kuamua kujiingiza katika maisha ya uteja ya utumiaji wa madawa ya kelevya.
Baada ya jitihada za familia yake aliweza kuondoka katika
maisha hayo ya uteja na alipo toka aliachia nyimbo za 'Bombokiata' na 'Mteja
Aliyepata Nafuu'.
Langa alizaliwa mnano mwaka 1985 jijini Dar es Salaam akiwa
tunda la wanandoa Vanessa Kimei na mumewe Mengisen Kileo.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Msingi Olympio na
baade Sekondari ya Loyola, zote za
jijini Dar es Salaam.
Akiwa kidato cha pili
alihamishiwa Kampala, Uganda katika Shule ya Vienna na baadaye Shule ya
Hillside International Academy, huko huko Uganda. Baadaye alirejea nchini na
kujiunga na masomo ya Stashahada ya Masoko katika Chuo cha Biashara Dar es
Salaam (CBE), Kampasi ya Dodoma.
No comments:
Post a Comment